Feb 9, 2012

LIKIZO

JUMUIYA YA WAISLAMU WA IFM (IMUS) INAWATAKIA LIKIZO NJEMA WANAJUMUIYA WOTE INSHALLAH TUTAONANA TENA SEMESTER IJAYO INSHALLAH

Jan 15, 2011

IMUS SUBSCRIPTION FEE!!!! JAMANI TUENDELEE KUCHANGIA JUMUIYA


Jumuiya ya waislamu wa IFM bado inaendelea kuwakumbusha wana-IMUS  wote kuharakisha kutoa ada ya uanachama(imus subscription fee) kwani hali ya uchangiaji inakatisha tamaa.Ikumbukwe kila mwaka, kila mwana-IMUS anatakiwa kuchangia kiasi cha TSh.14000/= kama ada ya mwaka mzima au TSh.7000/= kwa kila semista moja, lakini kwa mujibu wa Idara ya Fedha imus, hadi kufikia Januari  14- 2011, ni watu 16 tu waliokamilisha ada zao kati ya wanachama  zaidi ya 700.hali hii hairidhishi jamani ukizingatia pesa hizo ndiyo hutumika kuendeshea shughuli mbalimbali za IMUS kama kununua vitabu, viti, n.k. Hivyo Waislam tunaombwa tuongeze kasi ya kuchangia jumuiya yetu kwasababu mbali na kua ni sehemu ya Ibada ya kutoa(SADAKA), lakini pia ni wajibu wetu kwani suala hili ni kwa mujibu wa katiba ya IMUS.Hivyo kila mwana- Imus anatakiwa kuchangia bila kukosa.Ili kuchangia +255713 533 799
 ……”QUR’AN (63:10- 11)”